Vifaa vidogo rahisi kuchukua

Taa ya kusomea

Sahau kuhusu kiza wakati wa usiku na harufu ya mafuta ya taa or kubadili mshumaa. Sahau matumizi ya mara kwa mara ya mafuta ya taa na mishumaa. Kwa kununua mara moja tu taa hii ndogo nzuri kutaokoa matumizi fedha zako kwa miaka mingi ijayo.

Maelezo

  • Kigae cha jua: 3 W/5V
  • Betri: 3.2 V/400MAh LiFePO4
  • Taa: 0.5W LED bulb
  • Muda wa kuchaji: masaa 4-5

Muda wa kuangaza: masaa 24

Tochi inayo taa ya kusomea

Tochi ya mkononi inayoweza kusomea. Taa hii imeunganishwa na kujengewa kigae cha jua hivyo ni rahisi kutembea nayo au kuitumia kwa shughuli mbalimbali za nyumbani.

Maelezo

  • Kigae cha jua: 25W/5V
  • Betri: 3.2 V/250MAh LiFePO4
  • Taa: 0.5W LED bulb
  • Muda wa kuchaji: masaa 6-8
  • Muda wa kuangaza: masaa 18

Balbu (tungi) na tochi

Taa inayobebeka yenye kigae kidogo madhubuti cha jua kwa ajili ya kuchaji betri. Kifaa hiki ni bora katika namna nyingi tofauti. Kwanza inaweza kufanya kazi ya kutoa mwangaza. Lakini vile vile inaweza kufanya kazi ya kuchaji simu na kuitumia kama kihifadhi chaji ya akiba. Pia mna kebo au sehemu za kuchaji sim za aina tofauti.

Maelezo

  • Kigae cha jua: 0W/5.5V + 6m cable
  • Betri: 4,4VAh Lithium
  • Taa: 3W LED balbu lenye sehem 3 (3W, 2W, 1W)
  • Muda wa kuchaji: masaa 8 – 10
  • Muda wa kuangaza: 3W=masaa 6, 2W=masaa 10,1W=masaa 18
  • Kebo zimejumuishwa kwa ajili ya sim za aina tofauti